Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Chuo cha Taifa cha Ulinzi - Tanzania

Brig Gen Hassan Rashid Mabena
Mshiriki wa Kozi ya 13 kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ninajivunia kuwa mshiriki wa Kozi ya 13 ya NDC-TZ. Nimeona programu ya wiki 47 kuwa ya manufaa makubwa kwa taaluma yangu kama kiongozi wa kimkakati. Kwa kuzingatia zaidi mipango ya kimkakati na uamuzi, kozi hii imesaidia sana kuelewa usalama wa taifa kama mfumo jumuishi unaojumuisha nyanja za kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiteknolojia, kidiplomasia na kijeshi. Kupitia moduli zilizopangwa, mazoezi ya kimkakati, tafiti na mafunzo kwa vitendo, kozi hii imeniongezea uwezo wa kufikiri kwa kina na kufanya maamuzi kwa ufanisi. Mshikamano na wataalamu kutoka sekta mbalimbali umeongeza upeo wangu zaidi, na kunipa nguvu ya kuhudumia maslahi ya kijeshi na ya kitaifa kwa ufanisi
Mr. Batholomeo Kingolokele Jungu
Mshiriki wa Kozi ya 13 ya NDC-TZ kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mimi ni mhitimu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Tanzania kozi ya 13 Mwaka 2024/2025 (NDC-TZ), ninakiri kwa dhati kuwa chuo hiki ni taasisi ya kipekee, yenye mchango mkubwa na inayodhihirisha dhamira yake ya dhati katika kukuza ubora wa kitaaluma na maono ya kimkakati. Kimekuwa chombo muhimu katika kuwaandaa viongozi kwa utaalamu wa kimkakati wa kushughulikia changamoto ngumu za usalama wa taifa katika mazingira ya kimataifa yanayobadilika kwa kasi. Kupitia mafunzo katika chuo hiki, nimepata uzoefu wa kipekee na wa kina kuhusu mikakati ya usalama wa taifa, mazoezi ya kimkakati na uchambuzi wa sera kwa mtazamo wa jiografia ya kisiasa, ulinzi na usalama, utawala na maamuzi, uhusiano wa kimataifa na diplomasia. Mafunzo haya yamekuwa darasa la juu la kubadilishana uzoefu na mbinu bora kati ya wataalamu wa kiraia na kijeshi katika kufanikisha maendeleo ya taifa.
ACP Berthaneema Wilhelim Mlay
Mshiriki wa Kozi ya 13 kutoka Tanzania
Chuo cha Ulinzi cha Taifa cha Tanzania kinahudumu kama taasisi ya mageuzi, kikitoa maarifa ya thamani juu ya fikra za kimkakati, ushirikiano baina ya taasisi, na usalama wa kimataifa. Mtaala uliojaa kila aina ya maarifa, ukichangiwa na asili mbalimbali za washiriki, hujenga mazingira yenye msisimko wa kiakili na mijadala ya hali ya juu. Kupitia mihadhara ya kina, majadiliano, semina, na ziara za mafunzo ndani na nje ya nchi, chuo hiki huongeza kwa kiwango kikubwa uelewa kuhusu masuala ya usalama wa kitaifa, kikanda na kimataifa. Kozi hii ni hatua muhimu sana katika kitaaluma, kwani hutupatia mtazamo wa kimkakati na ujuzi wa uongozi unaohitajika ili kulihudumia taifa letu kwa ufanisi zaidi.
Colonel Kosgey Kimeli
Mshiriki wa Kozi ya Kumi na moja kutoka Kenya
Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (NDC-TZ) ni Taasisi inayoongoza kwa kuimarisha kipengele muhimu zaidi cha usalama wa Taifa. Chuo hiki kimekuwa ni kiungo muhimu katika kuhakikisha kwamba viongozi, watendaji wa usalama na wataalam wanakuwa bora ili kuendana na mienendo ya kimkakati kwa mazingira ya usalama na yanayobadilika kila mara.
Ms. Neema Mwakalyelye, ndc
Naibu Mkurugenzi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
‘Nikiri wazi kwamba wiki 47 nilizokaa NDC zimenipandisha kwenye kiwango cha juu cha ujuzi na uelewa wa wajibu wangu kama raia, mtumishi wa umma na kiongozi katika masuala ya usalama wa Taifa. Kozi imenifundisha kufikiri na kufanya mabo kwa njia tofauti. Kusema kweli nimejitolea zaidi kuona kwamba mikakati ya Serikali inalenga kuifanya Tanzaniakuwa mahali salama, sio tu kutokuwa na migogoroya ndani na vita bali pia kwa Tanzania kuwa sehemu ambayo fursa za ajira ni kubwa, watu wana afya njema, utawala bora unatekelezwa na amani ipo.’