Karibu
Ninayofuraha kuitambulisha kwenu na kuwakaribisha kwenye Tovuti ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi -Tanzania (NDC-TZ). Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2012, NDC-TZ imeendelea kuwa Chuo pekee chini ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kinachotoa Mafunzo ya Usalama na ya Kimkakati. NDC-TZ ni Taasisi ya Elimu ya Juu iliyosajiliwa na kuthibitishwa kikamilifu na Baraza la Taifa la Elimu na Ufundi Stadi (NACTVET). Hivyo, Pamoja na kutoa Tuzo ya Kifahari ya ‘ndc’ kwa Wahitimu wake, Chuo kina hadhi na mamlaka ya kutoa elimu ngazi ya Shahada ya Uzamili ya masomo ya Usalama na Kimkakati (MSSS) na Stashahada ya masomo ya Usalama na Kimkakati (DSSS) kutegemeana na ngazi ya elimu aliyonayo Mshiriki wa Kozi.
Tovuti hii inatoa taarifa kuhusu Chuo, Programu, Wafanyakazi na Utawala ili kukidhi matarajio ya Wasomaji. Chuo kimejikita katika kuleta ufahamu kuhusu maudhui na dhana halisi ya Usalama wa Taifa na Stratejia katika Kozi Ndefu na Fupi.
Ni Dhahiri kwamba tumeweza kutekeleza majukumu tuliyopewa kutokana na maoni yako wewe msomaji wa tovuti hii. Kwa muktadha huo, Chuo kinaomba wasomaji wa tovuti yetu waendelee kuitembelea na kutoa maoni yao kwa ustawi wa sasa na baadaye wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi-Tanzania.
Wilbert Augustin Ibuge, ndc
Meja Jenerali
Mkuu wa Chuo