Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Chuo cha Taifa cha Ulinzi - Tanzania

Ujumbe wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania ukiongozwa na Brigedia Jenerali CJ Ndiege – Mkufunzi Mwandamizi Elekezi Jeshi la Ardhini, umetembelea katika kampuni ya magari ya GF Vehicle Assembler Ltd wakati wa ziara ya kimafunzo mkoani Pwani tarehe 15 Januari 2025.